Karibu AfyaTrack

Mtandao pekee unaokupa taarifa, ushauri na huduma za afya ya mama na mtoto.

Taarifa
Web
Ushauri
App
Elimu
App/Web
Huduma
App/Web
Emergency number
+255 662 029 400
112
Piga namba hii kwa dharura ya afya, moto au polisi nchini Tanzania.

Historia fupi kuhusu AfyaTrack

Dr Winluck Shayo, Founder

“AfyaTrack-Tovuti” pamoja na “AfyaTrack-App” ni huduma mtandao zilizoanzishwa nchini Tanzania kuwakomboa wanawake na watoto wakiwa kama kundi maalumu la afya kwenye jamii. AfyaTrack imedhamiria kutoa taarifa, ushauri na huduma za afya kwa jamii kuhusu ujauzito, mtoto na malezi bora kwa lugha ya Kiswahili. Maamuzi ya kutumua Kiswahili ni ili kuweza kuwafikia walengwa kwa lugha nyepesi na inayoeleweka ili kuleta mapinduzi ya uhaba wa taarifa sahihi za afya na zinazopatikana kwa wakati sahihi mtandaoni.

Ifahamu AfyaTrack App

About Us
Kwa wajawazito na walezi wa watoto nchini Tanzania, AfyaTrack App ni application ya kwanza na tegemezi kutoa taarifa, ushauri na makala maalumu za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto wiki hadi wiki kwa lugha ya Kiswahili.

Maswali ya Mara kwa Mara

AfyaTrack App ni application ya simu za mkonnoni kama "Facebook" au "Instagram" inayokuwezesha kupata taarifa za maendeleo ya ujauzito au ukuaji wa mtoto wiki hadi wiki kwa lugha nyepesi ya Kiswahili. Unapopakua App hii na kuwa nayo kwenye simu yako una uhakika wa kupata taarifa na ushauri utakaoendana na umri wa ujauzito wako au mtoto wako kuhusu mabadiliko yako kimwili, mabadiliko yanayotokea kwa mtoto, lishe na vyakula, dalili hatarishi na vipimo maalumu, uhudhuriaji wa kliniki na chanjo husika, mazoezi na mapumziko, ukuaji wa mtoto na malezi bora na mengineyo mengi.
Application ya AfyaTrack inapatikana kirahisi sana. Kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa "Android" unachotakiwa kufanya ni kufungua app ya "Google Play Store" halafu unatafuta app ya AfyaTrack kwa kuandika maneno "AfyaTrack" kwenye sehemu ya kutafutia - search. Mara zote application itakayotokea ya kwanza ndio husika. Kisha unaipakua na hakikisha imeingia kwenye simu yako (Utahitaji kuwa na kifurushi cha kuperuzi mtandao kufanikisha hatua hii). Ukishafanikiwa kuiingiza kwenye simu yako hatua zinazofuata za kujiunga zinajieleza ukiifungua app.
AfyaTrack app inakupa uwezo wa kujiunga na huduma za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito wako au ukuaji wa mtoto wako. Ifahamike kwamba unaweza kujiunga na huduma moja kwa wakati mmoja. Unapoifungua app utapelekwa moja kwa moja kwenye sehemu ya kuingiza taarifa zako muhimu kama barua pepe, neno la siri nk. Ukifanikiwa kupita hatua hii, hatua inayofuata utaweza kuchagua huduma ya ufuatiliaji unayotaka kutumia, kati ya UJAUZITO au MTOTO. Ukichagua huduma ya Ujauzito utatakiwa kuingiza tarehe yako ya kwanza ya hedhi iliyopita ili application iweze kukupeleka moja kwa moja kuanza kupata taarifa za ujauzito kwa wiki uliyopo wakati huo. Ukichagua huduma ya Mtoto utahitajika kuingiza tarehe ya kuzaliwa ya mtoto husika ili uweze kupelekwa moja kwa moja kuanza kupata taarifa za ukuaji wa mtoto kwa wakati huo. (Kumbuka: Kwa sasa huduma ya ufuatiliaji ya ukuaji wa mtoto ni mpaka mtoto atakapofikisha mwaka mmoja pekee, tunaendelea kuongeza huduma hii ifike hadi miaka mitano na kuendelea)
BURE. App ya AfyaTrack haina malipo yoyote kuipakua au kujiunga kuweza kuitumia. Huduma hii inawezeshwa na mashirika mbali mbali yanayojali afya ya mama na mtoto kuifanya ipatikane bure bila malipo yoyote.

Vitengo

Taarifa

Pata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu afya ya mama na mtoto kutoka AfyaTrack Web na AfyaTrack App.

Huduma

Jiunge na huduma zetu za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa kupakua AfyaTrack App.

Ushauri

Pata ushauri wetu wa afya ya mama na mtoto toka kwa Madaktari wetu

Elimu

Pata mafunzo mbali mbali kwa kusoma makala zetu za afya zilizoandikwa na kupitiwa na wataalamu wetu wa afya.

Utafiti

Shiriki na soma kuhusu tafiti mbali mbali tunazofanya na kushirikishwa na mashirika mengine.

Dharura

AfyaTrack inakupa mwongozo na hatua za kuchukua pale unapopatwa na dharura.

AfyaTrack App

Fuatilia Maendeleo ya Ujauzito na Ukuaji wa Mtoto Wiki Hadi Wiki.

Blog Yetu

Kiungulia Wakati wa Ujauzito.

Kiungulia Wakati wa Ujauzito.

Kipindi cha ujauzito mabadiliko mbalimbali hutokea katika mwili wa mjamzito ili kuruhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto aliye tumboni, mabadiliko…

Kujifungua kwa Njia ya Kawaida Baada ya Kujifungua kwa Upasuaji (VBAC)

Kujifungua kwa Njia ya Kawaida Baada ya Kujifungua kwa Upasuaji (VBAC)

Ikiwa unajiuliza kama kujifungua kwa njia ya kawaida inawezekana baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji ujauzito uliopita, jibu ni…

Testimonials/Shuhuda

Ushauri wa Afya Toka kwa Wataalamu

Makala za kiafya zilizopo kwenye mtandao huu, pamoja na zile zilizopo kwenye application ya AfyaTrack zimeandikwa na kupitiwa na wataalamu wa afya. Hata hivyo ni vyema kutambua, ushauri unaoupata kwenye mitandao ni wa kuelimisha na kukupa uelewa wa taarifa mbalimbali za kiafya na sio vinginevyo. Unachokisoma kwenye mtandao huu hakitengui maamuzi ya daktrari ulipohudhuria au utakapohudhuria kituo chochote cha afya. Kwa maelezo zaidi soma:
1. Makala yetu ya sheria na taratibu za matumizi ya mtandao huu (Terms and Conditions)
2. Makala yetu ya usiri wa taarifa zako (Privacy Policy)