Mtoto wa umri huu:
- Anaweza kuvaa mwenyewe isipokuwa kufunga viatu.
- Anaweza kuruka na kutua na mguu mmoja.
- Anaweza kutupa mpira na kudaka.
- Anauliza maswali mengi na ana shahuku.
- Anaigiza wengine.
- Anatambua herufi na namba.
- Anaweza kuiga kuimba nyimbo, hadithi.
- Anashirikiana na wenzake kwenye michezo.
- Anasaidia watu nyumbani.
- Anaelewa hisia za watu wengine.
Ukuaji wa kimwili katika umri huu
- Anakomaa kiakili
- Anaweza kusimama na mguu mmoja bila kuyumba
- Anashuka ngazi bila kujishika
- Anakimbia na kusimama bila kuanguka
- Anaweza kuruka juu ya matofali na miguu yote bila kuanguka
- Anaweza kuruka urefu wa hatua tatu na kutua na miguu yote
Maendeleo ya mtoto katika jamii ndani ya miezi hii
- Anapenda kujitegemea lakini bado anatumia mda wake na wazazi wake.
- Mtoto aliye na miaka 5 anapenda kujihusisha na mengi, na mara nyingi atakataa msaada wako.
- Wanafanya usafi wenyewe, wakati mwingine bila kuamriwa.
- Wapenda kubembeleza wenzake hasa kama walihusika katika ugomvi.
- Wanaweza kujielezea wanavyohisi, mfano “huzuni, hasira, kuchanganyikiwa , uoga,kuvunjika moyo” n.k
- Wanakua kipaji cha kuwasiliana na kujadiliana na marafiki zake katika michezo yao.
- Wanaweza kuwa na rafiki mmoja kipenzi.
- Wana vipaji vingi vya kushirikiana na rafiki zake wengine.
- Wanashiriki katika kazi za vikundi shuleni na wanaweza kusubiria zamu yao kuongea au kufanya onyesho.
- Wazazi na walimu ni watu muhimu kwao, na chanzo cha habari na faraja.
- Wanaanza kufuata kanuni na sheria na wakati mwingine wanakumbusha wenzao, bila maelekezo ya mwalimu au mzazi.
Hatua za ukuaji katika kuongea na kujifunza
- Wanaelezea mahitaji, hisia, na mawazo yao.
- Wanapenda kupata habari zaidi.
- Wanafanya suluhisho la matatizo na kuchunguza mawazo yao.
- Wanafanya mipango ya vitu wanavyohitaji.
- Wanashauri wenzao na kutetea mada.
- Wanatengeneza na kuhadithia hadithi.